Pages

Wednesday, April 30, 2014

SHILOLE KUFUNGUA RASMI UKUMBI WA (THE CLUB HOUSE)






 KAUNTA INAENDELEA KUPANGWA VITU
 BAADHI YA SEHEMU ZA KUTULIA

 NURMAK KWA AJILI YA KAZI MOJA YA BURUDANI

 Dj ABUU FRESH Jr WA THE CLUB HOUSE AAHIDI VITU VIPYA KWA WAKAZI WA MUSOMA
MWANAMUZIKI ANAYEKUJA KWA KASI HAPA NCHINI SHILOLE "SHISH BEBY KESHO ANATARAJIWA KUTOA BURUDANI YA AINA YAKE KWA WAKAZI WA MJI WA MUSOMA IKIWA NI UZINDUZI RASMI WA UKUMBI WA KISASA WA THE CLUB HOUSE BAADA YA KUFANYIWA UKARABATI WA NGUVU.

AKIZUNGUMZA NA BLOG NDANI YA UKUMBI HUO,DJ MKUU WA CLUB HIYO ABUBAKAR NYAMAKATO DJ ABUU FRSH Jr AMESEMA MAANDALIZI YOTE YAMEKWENDA VIZURI KILICHOBAKI NI WAKAZI WA MUSOMA KUPATA BURUDANI YA AINA YAKE.

AMESEMA SHILOLE AKIWA NA KUNDI LAKE ZIMA LA WACHEZA SHOW AMEIPANIA SHOW HIYO KWA KUFANYA VIZURI ILI KUJENGA JINA ZURI KWA MASHABIKI WAKE AMBAO KWA KIASI KIKUBWA WAMETOKEA KUMUUNGA MKONO.

Dj ABUU AMESEMA KIINGILIO KWENYE SHOW HIYO YA AINA YAKE ILIYODHAMINIWA NA WADAU MBALIMBALI WA BURUDANI IKIWEMO BROG HII KITAKUWA SHILINGI 7000 HUKU SHOW IKITARAJIWA KUANZA MAPEMA SAA 2 USIKU NA KUOMBA WAPENZI WA BURUDANI KUJITOKEZA KWA WINGI. 

Tuesday, April 29, 2014

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI‏

 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi

Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.

Wednesday, April 23, 2014

AMWAGA RADHI SHOW YA FM ACADEMIA MUSOMA JIONEE HAPA



 MASHABIKI WA BURUDANI MUSOMA WAKIFATILIA SHOW YA FM ACADEMIA USIKU WA JANA BWALO LA MAGEREZA MUSOMA

 KAZI ILIANZA KIUNO MAUNO

 ALI NYOGA MAUNO KATIKA!.

 MCHAKAMCHAKA

 AMKA TUCHEZE WW




 FULL NGWASUMA

 NYOSHI AKIMCHEZESHA MNENGUAJI WAKE

 MKUBWA ABASI CHAMBA AKIWA NA NYOSHI EL SADAT

 JAMAA ALIWEKA GONGO LAKE PEMBENI IKAPINGWA NGWASUMA!



Tuesday, April 15, 2014

KAPOTIVE STAR SINGERS-BUKOBA KUFANYA TAMASHA LA PASAKA LINA'S CLUB, PASAKA PILI NI KATIKA MJI WA BIHARAMULO

Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers- Bukoba,Wanayo furaha kuwatangazia kuwa kwa mapenzi ya Mungu, Tar. 20/04/2014 sikukuu ya Pasaka watakuwa na tamasha la Pasaka LINA’S CLUB -Bukoba, kuanzia saa 9 mchana hadi 2 usiku na kesho yake tar. 21/04/2014 Watakuwa katika mji wa Biharamulo. 


 Mratibu wa Tamasha hilo Bw. Andrew Kagya amesema kuwa Mwimbaji mgeni (Guest singer) atakuwa Flora Mbasha na kundi lake zima kutoka jijini Dar es Salaam na pia Kutakuwepo kwaya mbalimbali za RC, KKKT na SDA za hapa Bukoba.Kiingilio kitakuwa kama ifuatavyo:Mtu mmoja 10,000/-

Watu watatu  25,000/-,  Watoto 5,000/-
Kutokana na udhamini wa kinywaji maridadi cha Climax Non-Alcoholic Herbal drink, kila atakayenunua ticket ya 10,000, atapewa kinywaji kimoja cha Climax mlangoni, na atakayenunua ticket ya 25,000 atapewa CD moja mpya ya KAPOTIVE Star Singers (Zawadi ya Pasaka) na vinywaji vitatu vya Climax bure. Karibuni tusherekee ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristu kwa nyimbo na shangwe.Baadhi ya waimbaji wa Kapotive Star wakiimba kwenye matamasha yao yaliyopitaKazaliwa!! Njoo mumuone!!