Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kayombo intertainment,docta Kayombo aaamesema baada ya kupata mafanikio kwenye show ya usiku wa valentine day ndani ya bwalo la polisi mjini Musoma sasa ameamua kuandaa utaratibu wa kuwapa burudani wakazi wa Musoma na mkoa wa Mara kwa ujumla kila mara.
Akizungumza na blog hii,Kayombo amesema kutokana na watu walivyopokea show hiyo anaamini wakazi wa musoma licha ya kujishughulisha na shughuli zao za kiuchumi baada ya kazi wanapenda kujipumzisha na kupata burudani.
Amesema kwa sasa baada ya kuagiza na kufika vyombo vya kisasa vya muziki kilichobaki ni kuhakikisha wakazi wa musoma na vitongoji vyake wanapata burudani nzuri wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki
No comments:
Post a Comment