Pages

Friday, February 28, 2014

MAKOMANDOO,WAZEE WA KIBABA BABA KUPAGAWAISHA BWALO LA POLISI MUSOMA KESHO




Kundi linaloongoza kwa sasa kufanya show kali na kupagawisha watanzamaji kwa kuimba na kuicheza la makomandoo kutoka jijini Dar es salaam linatarajiwa kufanya show kali katika miji ya Musoma,Tarime na Shirati mkoani Mara.

Akizungumza na shommi Blog,muandaaji wa show ambaye pia ni mkurugenzi wa Kayombo Intertainment,Docta Kayombo amesema kwa sasa tayari wasanii hao wameshawasili mjini Musoma tayari kwa kuanza kutoa burudani kwa wakazi wa maeneo hayo.

Kayombo amesema kama ambayo aliwaahidi wakazi wa Musoma na maeneo mengine ya mkoa wa Mara katika show ya usiku wa valentine day ni kuhakikisha wapenzi wa burudani wanapata burudani kila mwishoni mwa wiki baada ya shughuli za kazi.

Amesema show ya kwanza kundio hilo la makomandoo ambalo litasindikizwa na wasanii wengine wakali wa mkoa wa Mara jumamosi ya tarehe 22 watafanya show ya kwanza kwenye ukumbi wa JJ mjini Tarime kabla ya jumapili kufanya show mjini Musoma kwenye ukumbi wa bwalo la polisi klabla ya kumalizia show mjini Shirati jumatatu.

Kayombo amesema baada ya show hiyo ya makomandoo wakazi wa Musoma na maeneo mengine ya mkoa wa Mara watarajie show za wasanii wengine wakali ambao kila wakati watakuwa wakija kutoa burudani kama ilivyo kwenye maeneo mengine.

Saturday, February 15, 2014

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA VALENTINE DAY MUSOMA NA KAYOMBO INTERTAINMENT MDANI YA BWALO LA POLISI

 FULL KUJIACHIA
 NI BATA
 ANATAFUTWA MR NA MISS VALANTINE DAY KWA AJILI YA KUJINYAKULIA MPUNGA WA 50,000
 MR VALENTINE AKIFURAHI NA WAPAMBE WAKE

 MSHINDI WA BSS 2013 EMANUEL MSUYA AKITOA BURUDANI
 

 KAYOMBO INTERTAINMENT CLEW
 DOCTA KAYOMBO AKIWA NA MHAZINI MKUU WA KAMPUNI NA KICHUPA MKONONI
 UFATILIAJI
 NIKO NA MKURUGENZI MKUU WA BURUDANI MUSOMA
 MSUYA AKITOA MPUNGA KWA MISS VALENTINE
MPUNGA PIA ULIMUHUSU MR VALENTINE

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kayombo intertainment,docta Kayombo aaamesema baada ya kupata mafanikio kwenye show ya usiku wa valentine day ndani ya bwalo la polisi mjini Musoma sasa ameamua kuandaa utaratibu wa kuwapa burudani wakazi wa Musoma na mkoa wa Mara kwa ujumla kila mara.

Akizungumza na blog hii,Kayombo amesema kutokana na watu walivyopokea show hiyo anaamini wakazi wa musoma licha ya kujishughulisha na shughuli zao za kiuchumi baada ya kazi wanapenda kujipumzisha na kupata burudani.

Amesema kwa sasa baada ya kuagiza na kufika vyombo vya kisasa vya muziki kilichobaki ni kuhakikisha wakazi wa musoma na vitongoji vyake wanapata burudani nzuri wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki

Tuesday, February 11, 2014

USIKU WA DAYNA NYANGE TZ V/S CINDY SANYU WA UG NDANI YA LINAS NIGHT CLUB BUKOBA FEB 15, 2014


FEB 15, 2014 Itakuwa ni usiku wa aina yake kwa wakazi wa mji wa Bukoba na maeneo ya jirani, Watakapo takiwa kujua nani mkali kati ya DAYNA NYANGE TZ V/S CINDY SANYU WA UG .Usiku huo hatuangalii Vivazi au  nani anamiliki nini,ama yupi ni hot zaidi ya mwenzake,tunaangalia kitu kimoja tu,Nani mkali wa kuimba na kucheza Jukwaani?