Pages

Sunday, September 7, 2014

PICHA 30 ZA SHOW YA FIESTA MUSOMA,NI SHIDAAAAAAA..................

7
 Serengeti Fiesta September 7 2014 Musoma, show ambayo ilifanywa maalum baada ya maamuzi kufikiwa ili upendo usambazwe kwa wote waliofiwa na waliojeruhiwa kwenye ajali ya Mabasi iliyoua 39 Musoma September 5 2014.Show ilikua ifanyike Ijumaa lakini iliahirishwa siku hiyohiyo baada ya ajali kutokea na ilikua isifanyike moja kwa moja, Jumamosi watu ikiwa ni pamoja na Wasanii wakiwa wamejiandaa na safari, stage kianza kuondolewa ili kusafirishwa…. likaja wazo kwamba inaweza kufanyika show ya Fiesta lakini ikawa maalum kwa ajili ya ajali ya Ijumaa.
6
2
3

Saturday, August 16, 2014

TAZAMA PICHA 15 ZA SHOW YA FIESTA BUKOBA,NI NOMAAA WAHAYA WARUKA RUKAAAAA

Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki(kushoto) ndie alikuwa Mgeni rasmi  katika Tamasha la Serengeti fiesta 2014 katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Tamasha limefanyika usiku wa kuamkia leo. Viongozi mbalimbali wa Serikali, Pamoja na Wananchi mbalimbali walihudhulia kwa wingi katika Uwanja huo wa Kaitaba. katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoa Mheshimiwa Zipporah Pangani na kulia ni Bw. Denis.Mkurugenzi wa Vipindi, Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group, Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na kumkaribisha Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki jukwaani na kusalimiana na Wakazi wa Bukoba waliokuwa kwenye Tamasha hilo la Serengeti Fiesta 2014 kwenye Uwanja wa Kaitaba.


Friday, May 2, 2014

HIVI NDIVYO SHILOLE AIVYOZINDUA RASMI UKUMBI WA THE CLUB HOUSE MJINI MUSOMA ILIKUWA BALAAAAA JIONEE HAPA




 
 Dj TIMBA AIWAPAGAWISHA MASHABIKI NDANI YA THE CLUB HOUSE
 THE CLUB HOUSE UNAWEZA UKAFATILIA SHOW UIWA CHINI AMA JUU
 Djs TIMBA NA ABUU FRESH Jr WA THE CLUB HOUSE
 DANSA WA SHILOLE
 NI MWENDO WA BURUDANI



 SHILOLE AKIWARUSHA MASHABIKI

 HAPA NI BURUDANI TU.
 YALAAH!


Wednesday, April 30, 2014

SHILOLE KUFUNGUA RASMI UKUMBI WA (THE CLUB HOUSE)






 KAUNTA INAENDELEA KUPANGWA VITU
 BAADHI YA SEHEMU ZA KUTULIA

 NURMAK KWA AJILI YA KAZI MOJA YA BURUDANI

 Dj ABUU FRESH Jr WA THE CLUB HOUSE AAHIDI VITU VIPYA KWA WAKAZI WA MUSOMA
MWANAMUZIKI ANAYEKUJA KWA KASI HAPA NCHINI SHILOLE "SHISH BEBY KESHO ANATARAJIWA KUTOA BURUDANI YA AINA YAKE KWA WAKAZI WA MJI WA MUSOMA IKIWA NI UZINDUZI RASMI WA UKUMBI WA KISASA WA THE CLUB HOUSE BAADA YA KUFANYIWA UKARABATI WA NGUVU.

AKIZUNGUMZA NA BLOG NDANI YA UKUMBI HUO,DJ MKUU WA CLUB HIYO ABUBAKAR NYAMAKATO DJ ABUU FRSH Jr AMESEMA MAANDALIZI YOTE YAMEKWENDA VIZURI KILICHOBAKI NI WAKAZI WA MUSOMA KUPATA BURUDANI YA AINA YAKE.

AMESEMA SHILOLE AKIWA NA KUNDI LAKE ZIMA LA WACHEZA SHOW AMEIPANIA SHOW HIYO KWA KUFANYA VIZURI ILI KUJENGA JINA ZURI KWA MASHABIKI WAKE AMBAO KWA KIASI KIKUBWA WAMETOKEA KUMUUNGA MKONO.

Dj ABUU AMESEMA KIINGILIO KWENYE SHOW HIYO YA AINA YAKE ILIYODHAMINIWA NA WADAU MBALIMBALI WA BURUDANI IKIWEMO BROG HII KITAKUWA SHILINGI 7000 HUKU SHOW IKITARAJIWA KUANZA MAPEMA SAA 2 USIKU NA KUOMBA WAPENZI WA BURUDANI KUJITOKEZA KWA WINGI. 

Tuesday, April 29, 2014

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI‏

 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi

Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.

Wednesday, April 23, 2014

AMWAGA RADHI SHOW YA FM ACADEMIA MUSOMA JIONEE HAPA



 MASHABIKI WA BURUDANI MUSOMA WAKIFATILIA SHOW YA FM ACADEMIA USIKU WA JANA BWALO LA MAGEREZA MUSOMA

 KAZI ILIANZA KIUNO MAUNO

 ALI NYOGA MAUNO KATIKA!.

 MCHAKAMCHAKA

 AMKA TUCHEZE WW




 FULL NGWASUMA

 NYOSHI AKIMCHEZESHA MNENGUAJI WAKE

 MKUBWA ABASI CHAMBA AKIWA NA NYOSHI EL SADAT

 JAMAA ALIWEKA GONGO LAKE PEMBENI IKAPINGWA NGWASUMA!



Tuesday, April 15, 2014

KAPOTIVE STAR SINGERS-BUKOBA KUFANYA TAMASHA LA PASAKA LINA'S CLUB, PASAKA PILI NI KATIKA MJI WA BIHARAMULO

Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers- Bukoba,Wanayo furaha kuwatangazia kuwa kwa mapenzi ya Mungu, Tar. 20/04/2014 sikukuu ya Pasaka watakuwa na tamasha la Pasaka LINA’S CLUB -Bukoba, kuanzia saa 9 mchana hadi 2 usiku na kesho yake tar. 21/04/2014 Watakuwa katika mji wa Biharamulo. 


 Mratibu wa Tamasha hilo Bw. Andrew Kagya amesema kuwa Mwimbaji mgeni (Guest singer) atakuwa Flora Mbasha na kundi lake zima kutoka jijini Dar es Salaam na pia Kutakuwepo kwaya mbalimbali za RC, KKKT na SDA za hapa Bukoba.Kiingilio kitakuwa kama ifuatavyo:Mtu mmoja 10,000/-

Watu watatu  25,000/-,  Watoto 5,000/-
Kutokana na udhamini wa kinywaji maridadi cha Climax Non-Alcoholic Herbal drink, kila atakayenunua ticket ya 10,000, atapewa kinywaji kimoja cha Climax mlangoni, na atakayenunua ticket ya 25,000 atapewa CD moja mpya ya KAPOTIVE Star Singers (Zawadi ya Pasaka) na vinywaji vitatu vya Climax bure. Karibuni tusherekee ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristu kwa nyimbo na shangwe.Baadhi ya waimbaji wa Kapotive Star wakiimba kwenye matamasha yao yaliyopitaKazaliwa!! Njoo mumuone!!


Friday, February 28, 2014

MAKOMANDOO,WAZEE WA KIBABA BABA KUPAGAWAISHA BWALO LA POLISI MUSOMA KESHO




Kundi linaloongoza kwa sasa kufanya show kali na kupagawisha watanzamaji kwa kuimba na kuicheza la makomandoo kutoka jijini Dar es salaam linatarajiwa kufanya show kali katika miji ya Musoma,Tarime na Shirati mkoani Mara.

Akizungumza na shommi Blog,muandaaji wa show ambaye pia ni mkurugenzi wa Kayombo Intertainment,Docta Kayombo amesema kwa sasa tayari wasanii hao wameshawasili mjini Musoma tayari kwa kuanza kutoa burudani kwa wakazi wa maeneo hayo.

Kayombo amesema kama ambayo aliwaahidi wakazi wa Musoma na maeneo mengine ya mkoa wa Mara katika show ya usiku wa valentine day ni kuhakikisha wapenzi wa burudani wanapata burudani kila mwishoni mwa wiki baada ya shughuli za kazi.

Amesema show ya kwanza kundio hilo la makomandoo ambalo litasindikizwa na wasanii wengine wakali wa mkoa wa Mara jumamosi ya tarehe 22 watafanya show ya kwanza kwenye ukumbi wa JJ mjini Tarime kabla ya jumapili kufanya show mjini Musoma kwenye ukumbi wa bwalo la polisi klabla ya kumalizia show mjini Shirati jumatatu.

Kayombo amesema baada ya show hiyo ya makomandoo wakazi wa Musoma na maeneo mengine ya mkoa wa Mara watarajie show za wasanii wengine wakali ambao kila wakati watakuwa wakija kutoa burudani kama ilivyo kwenye maeneo mengine.