Friday, May 2, 2014
Wednesday, April 30, 2014
SHILOLE KUFUNGUA RASMI UKUMBI WA (THE CLUB HOUSE)
KAUNTA INAENDELEA KUPANGWA VITU
BAADHI YA SEHEMU ZA KUTULIA
NURMAK KWA AJILI YA KAZI MOJA YA BURUDANI
Dj ABUU FRESH Jr WA THE CLUB HOUSE AAHIDI VITU VIPYA KWA WAKAZI WA MUSOMA
MWANAMUZIKI ANAYEKUJA KWA KASI HAPA NCHINI SHILOLE "SHISH BEBY KESHO ANATARAJIWA KUTOA BURUDANI YA AINA YAKE KWA WAKAZI WA MJI WA MUSOMA IKIWA NI UZINDUZI RASMI WA UKUMBI WA KISASA WA THE CLUB HOUSE BAADA YA KUFANYIWA UKARABATI WA NGUVU.
AKIZUNGUMZA NA BLOG NDANI YA UKUMBI HUO,DJ MKUU WA CLUB HIYO ABUBAKAR NYAMAKATO DJ ABUU FRSH Jr AMESEMA MAANDALIZI YOTE YAMEKWENDA VIZURI KILICHOBAKI NI WAKAZI WA MUSOMA KUPATA BURUDANI YA AINA YAKE.
AMESEMA SHILOLE AKIWA NA KUNDI LAKE ZIMA LA WACHEZA SHOW AMEIPANIA SHOW HIYO KWA KUFANYA VIZURI ILI KUJENGA JINA ZURI KWA MASHABIKI WAKE AMBAO KWA KIASI KIKUBWA WAMETOKEA KUMUUNGA MKONO.
Dj ABUU AMESEMA KIINGILIO KWENYE SHOW HIYO YA AINA YAKE ILIYODHAMINIWA NA WADAU MBALIMBALI WA BURUDANI IKIWEMO BROG HII KITAKUWA SHILINGI 7000 HUKU SHOW IKITARAJIWA KUANZA MAPEMA SAA 2 USIKU NA KUOMBA WAPENZI WA BURUDANI KUJITOKEZA KWA WINGI.
Tuesday, April 29, 2014
FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi
Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani
Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.
Wednesday, April 23, 2014
AMWAGA RADHI SHOW YA FM ACADEMIA MUSOMA JIONEE HAPA
MASHABIKI WA BURUDANI MUSOMA WAKIFATILIA SHOW YA FM ACADEMIA USIKU WA JANA BWALO LA MAGEREZA MUSOMA
KAZI ILIANZA KIUNO MAUNO
ALI NYOGA MAUNO KATIKA!.
MCHAKAMCHAKA
AMKA TUCHEZE WW
FULL NGWASUMA
NYOSHI AKIMCHEZESHA MNENGUAJI WAKE
MKUBWA ABASI CHAMBA AKIWA NA NYOSHI EL SADAT
JAMAA ALIWEKA GONGO LAKE PEMBENI IKAPINGWA NGWASUMA!
Tuesday, April 15, 2014
KAPOTIVE STAR SINGERS-BUKOBA KUFANYA TAMASHA LA PASAKA LINA'S CLUB, PASAKA PILI NI KATIKA MJI WA BIHARAMULO
Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers- Bukoba,Wanayo furaha kuwatangazia kuwa kwa mapenzi ya Mungu, Tar. 20/04/2014 sikukuu ya Pasaka watakuwa na tamasha la Pasaka LINA’S CLUB -Bukoba, kuanzia saa 9 mchana hadi 2 usiku na kesho yake tar. 21/04/2014 Watakuwa katika mji wa Biharamulo.
Mratibu wa Tamasha hilo Bw. Andrew Kagya amesema kuwa Mwimbaji mgeni (Guest singer) atakuwa Flora Mbasha na kundi lake zima kutoka jijini Dar es Salaam na pia Kutakuwepo kwaya mbalimbali za RC, KKKT na SDA za hapa Bukoba.
Kiingilio kitakuwa kama ifuatavyo:Mtu mmoja 10,000/-
Watu watatu 25,000/-, Watoto 5,000/-
Kutokana na udhamini wa kinywaji maridadi cha Climax Non-Alcoholic Herbal drink, kila atakayenunua ticket ya 10,000, atapewa kinywaji kimoja cha Climax mlangoni, na atakayenunua ticket ya 25,000 atapewa CD moja mpya ya KAPOTIVE Star Singers (Zawadi ya Pasaka) na vinywaji vitatu vya Climax bure. Karibuni tusherekee ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristu kwa nyimbo na shangwe.Friday, February 28, 2014
MAKOMANDOO,WAZEE WA KIBABA BABA KUPAGAWAISHA BWALO LA POLISI MUSOMA KESHO



Akizungumza na shommi Blog,muandaaji wa show ambaye pia ni mkurugenzi wa Kayombo Intertainment,Docta Kayombo amesema kwa sasa tayari wasanii hao wameshawasili mjini Musoma tayari kwa kuanza kutoa burudani kwa wakazi wa maeneo hayo.
Kayombo amesema kama ambayo aliwaahidi wakazi wa Musoma na maeneo mengine ya mkoa wa Mara katika show ya usiku wa valentine day ni kuhakikisha wapenzi wa burudani wanapata burudani kila mwishoni mwa wiki baada ya shughuli za kazi.
Amesema show ya kwanza kundio hilo la makomandoo ambalo litasindikizwa na wasanii wengine wakali wa mkoa wa Mara jumamosi ya tarehe 22 watafanya show ya kwanza kwenye ukumbi wa JJ mjini Tarime kabla ya jumapili kufanya show mjini Musoma kwenye ukumbi wa bwalo la polisi klabla ya kumalizia show mjini Shirati jumatatu.
Kayombo amesema baada ya show hiyo ya makomandoo wakazi wa Musoma na maeneo mengine ya mkoa wa Mara watarajie show za wasanii wengine wakali ambao kila wakati watakuwa wakija kutoa burudani kama ilivyo kwenye maeneo mengine.
Saturday, February 15, 2014
HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA VALENTINE DAY MUSOMA NA KAYOMBO INTERTAINMENT MDANI YA BWALO LA POLISI
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kayombo intertainment,docta Kayombo aaamesema baada ya kupata mafanikio kwenye show ya usiku wa valentine day ndani ya bwalo la polisi mjini Musoma sasa ameamua kuandaa utaratibu wa kuwapa burudani wakazi wa Musoma na mkoa wa Mara kwa ujumla kila mara.
Akizungumza na blog hii,Kayombo amesema kutokana na watu walivyopokea show hiyo anaamini wakazi wa musoma licha ya kujishughulisha na shughuli zao za kiuchumi baada ya kazi wanapenda kujipumzisha na kupata burudani.
Amesema kwa sasa baada ya kuagiza na kufika vyombo vya kisasa vya muziki kilichobaki ni kuhakikisha wakazi wa musoma na vitongoji vyake wanapata burudani nzuri wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki
Subscribe to:
Posts (Atom)